• peterngumba 10w

  MUNKARI MALAIKA WA KIFO

  Kifo huishi na sisi, kama hewa tunavuta.
  hutwandama kama kesi, lengo kutukamata.
  Kifo kinatuandama, kama macho ya adui.

  Watu Nimeshuhudia , tulioanza na wao.
  Washindwa kumalizia, ndoto waloanza zao.
  Kifo kinatuandama, kama macho ya adui.

  Siku moja utamaka, ukamkia mbinguni.
  Badala ya kwako kaka, na uage duniani.
  Kifo kinatuandama, kama macho ya adui.

  Hutatupa na kwaheri, utatwachia majonzi.
  Utatamani ni heri, ungefanya nasi shenzi.
  Kifo kinatuandama, kama macho ya adui.

  Utakwenda futi sita, huko uliwe na mchwa.
  Na mwishowe saa sita, turudi makwetu, sawa.
  Kifo kinatuandama, kama macho ya adui.
  @peshphotographyke