• jerrumani 51w

  #Apc.
  #Jerryhoodpix.
  #worldstartfromthehood
  #swahilipoems
  Tag yourself and i consider you a fam.
  Contact me if you're interested whatsApp +255765868400
  #Tanzania

  Read More

  GARI BOVU

  Liko hovyo laegeshwa halitembei.
  Vioo kibogoyo wala sili kebehi.
  Seraze mboyoyo kusema sizembei.
  Hili gari letu sote pamoja tulikomboe

  Lina mafuta japo halitumii.
  Lima ufuta vita vya uchumi.
  Aheri guta kweli sitanii
  Hili gari letu sote pamoja tulikomboe

  Dereva aendesha akilitengeneza.
  Abiria waliegesha wakilibeza.
  Suria ajishibisha mlo wakingereza.
  Hili gari letu sote pamoja tulikomboe.

  Ankara ya tiba haifiki.
  Barabara ya diba haipitiki.
  Imara ni honda, habari kiki.
  Hili gari letu sote pamoja tulikomboe.

  Tairi vipara ona buzwagi.
  Injini mtwara, korosho sio bangi.
  Sevis shubiri kwara sivae wigi.
  Hili gari letu sote pamoja tulikomboe.

  Pembejeo pembe za ndovu ndo zao.
  Kende koleo kovu tia limao.
  Mambo leo tamaduni ovu kibao.
  Hili gari letu sote Pamoja tulikomboe

  Mshaara wa dhambi mauti.
  Masihara vitambi na gauti.
  Uchwara vumbi na nishati.
  Hili gari letu sote pamoja tulikomboe.

  Halinisitiri laniaibisha, fahari ya africa.
  Utitiri kubahatisha, lazidiwa na la nyika.
  Ata la jangwani nakiri japo tuna pilika.
  Hili gari letu sote pamoja tulikomboe

  Injini dhahabu stelingi tanzanite.
  Kiswahili tabu taskia gud naiti.
  Kuandikiwa vitabu si ndo manati?
  Hili gari letu sote pamoja tulikomboe

  Mabadiliko huanza na mimi.
  Maandiko hufunza yamkini.
  Uliko ukichunguza utabaini.
  Hili gari letu sote pamoja tulikomboe
  ©jerrymantzlengai