• sahihi_ya_mfalme 21w

  YA DUNIA

  Shehe Mstaarabu
  wajiita mmiliki, kwa kuwa we mtahiki
  wasema mwenye haki, kwa kuwa wajua mashtahiki
  wasema umetamalaki, waenda kote mashariki
  Ubaya uzuri havijitangazi, yote ya dunia.

  Sahihi ya Mfalme
  Ubeti huu nautunga, hino ni uhalisiya
  Sikupingi nakuunga, 'mepotea duniya
  Sijui yupi 'taichonga, kil'o hiki subiriya
  Maisha yaboronga, yote haya duniya

  Shehe Mstaarabu
  Makini tajazingatia, muhimu uhalisia
  Walo chini tawatia, hadhi kishtahikia
  Magharibi tatembelea, kote tawashikilia
  Kweli maishaa yaboronga, yote ya dunia

  Sahihi ya Mfalme
  Haijabadili muundo, ule ule tul'ostahili
  Mepoteza mwenendo, sijui ipi mithili
  Watu hayawani vitendo, utu hawastahimili
  Maisha yaboronga, yote haya duniya

  Shehe Mstaarabu
  Madhabauni wapanda, mishikiki wasifia
  Mashizi walea, fundo lisilofikia
  Hapa kule watakabalia , 'sahau lebekia
  Maisha yaboronga, yachoma dunia

  Sahihi ya Mfalme
  Nakubali un'osema hino, yalegeza tukisonga
  Tumebaki kulilia wino, tun'oabudu vipanga
  Tumeisha nguvu viuno, awali tuliopanga
  Maisha yaboronga, yote haya duniya

  Shehe Mstaarabu
  Mienendo mekuwa, kama kunguru
  Wakwao hawasemeki, nguvu 'metumalizia
  Nadhani shubiri, nyongo katiwa maliwito
  Kweli maisha meborongwa, haya yaani dunia

  Sahihi ya Mfalme
  Sahihi mimi natiwa, hapa mwisho nakomea
  Yaniliza kifikiriwa, ya dunia al'otutengea
  Nisije hukumiwa, machafu mtu nasemea
  Ya Mfalme Sahihi nimetiwa, fulisitopu hapa natia.

  Shehe Mstaarabu
  Tamati 'mefika, Shehe langu jina
  Kibwagizo tawacha, kesho giza
  vyema fikiri kwanza, wema si mwema
  Shehe Mstarabu, mbele tasonga leo natarajia


  Na: Kadima Emmanuel (Sahihi ya Mfalme)

  Lennox Caleb (Shehe Mstaarabu)